TSH BIL 14 KUHIFADHI CHAKULA TANI 28,000
KATAVI
Kiasi cha shilingi bilioni 14 kimetolewa na serikali ya awamu ya sita kwa wizara ya kilimo kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa ajili ya kujenga vihenge na maghala ya kisasa ya kuhifadhia chakula katika manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi hatua itakayongeza kuhifadhi nafaka kutoka tani 5,000 za sasa hadi tani 28,000.
“Mradi huu wenye thamani ya shilingi bilioni 14, utasaidia nchi kukabiliana na uhaba wa chakula na kupunguza upotevu wa baada ya mavuno. Maghala ya kisasa yameongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 5,000 hadi tani 28,000,” Dkt Samia amesema.
Aidha Dkt Samia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka ili kufikia tani milioni tatu ifikapo mwaka 2030.