TSH BIL 34 KUJENGA KITUO OSBP MANYOVU
KIGOMA.
Kiasi cha Shilingi bilioni 34 kimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha pamoja cha Forodha (One Stop Boarder Post- OSBP) katika eneo la Manyovu Mkoani Kigoma ambapo ni mpaka kati ya Tanzania na Burundi ili kuwezesha Mkoa wa Kigoma kufanya biashara na nchi jirani.
Kituo hicho kitakuwa cha kisasa na kikikamilika kitasaida kuboresha biashara na kuwezesha Mkoa wa Kigoma kuwa kitovu cha biashara kwa nchi yetu na nchi za jirani za Burundi na DRC (Congo)
Katika kufanikisha azma hiyo serikali itahakikisha Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Fedha inawalipa fidia wananchi watakaopisha ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha kiasi cha Shilingi Bilioni 1.7 kabla ya kuanza kwa ujenzi wa kituo hicho.