TSH TRIL 1.2 KUIBORESHA NGUVU MUHIMBILI
DAR ES SALAAM
Serikali imedhamiria kuboresha Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuijenga upya ili kuwezesha huduma zote kutolewa ndani ya jengo moja litakalokuwa na vitanda 1,757 kutoka 1,435 vya sasa ambapo mradi huo utagharimu USD .468 Mil (takribani TZS. 1.2 Trilioni) ambapo kati ya fedha hizo USD.364 Mil zitatoka Korea Kusini na Serikali ya Tanzania itachangia USD. 104 Mil.
Utekelezaji wa mradi huo ni wa awamu moja ambao utachukua miaka mitano kukamilika baada ya kusaini mkataba, hatua hii haitaathiri utoaji wa huduma hospitalini hapa hivyo huduma zitaendelea kutolewa kama kawaida.
Aidha, mradi huu wa kihistoria katika sekta ya afya nchini na Ukanda wa Afrika, utakuwa na faida lukuki ikiwemo kuboreshwa kwa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi kupitia vifaa tiba vya kisasa na kwamba Serikali itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya fedha kusafirisha wagonjwa nje ya nchi, kuwezesha wagonjwa kupata huduma zote katika eneo moja, kupunguza mizunguko na usumbufu pamoja na kuwa na mpangilio mpya wa hospitali huku eneo kubwa likibaki wazi kwa matumizi ya maendeleo mengine miaka 50 ijayo