UPATIKANAJI WA MAJI SAFI BUNDA SASA NI 85%
MARA
Katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa Dkt Samia serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) imefanikiwa kuongeza huduma ya maji kwa wananchi kwa asilimia 85 huku matarajio yakiwa kuvuka lengo la ilani ya CCM 2020-2025 (Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 imeweka lengo la kufikia 95% ya maji mijini na 85% vijijini ifikapo mwisho wa 2025.)Mafanikio hayo makubwa yametokana na mgao wa kibajeti unaotolewa na serikali ya awamu ya sita, ambao umewezesha utekelezaji wa miradi imara ya maji katika jimbo la Bunda mkoani Mara.