DKT SAMIA AOKOA MAISHA YA WATOTO 20 WENYE SELIMUNDU

 

DKT SAMIA AOKOA MAISHA YA WATOTO 20 WENYE SELIMUNDU

DKT SAMIA AOKOA MAISHA YA WATOTO 20 WENYE SELIMUNDU

DODOMA 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameokoa maisha ya watoto 20 waliokuwa na ugonjwa wa selimundu ambao kupitia mfuko maalum wa Mhe Rais Samia walipandikizwa uloto na wamepona.
Huduma hiyo ilitumia Sh bilioni 1.1 iliyotolewa kupitia Mfuko Maalumu wa Rais Samia Suluhu Hassan na kama watoto hao wangepatiwa huduma hiyo nje ya nchi, ingetumika Sh bilioni 2.1 hivyo Sh bilioni moja  imeokolewa.
Katika kipindi cha miaka minne ya Rais Samia, uvunaji wa figo katika hospitali hiyo umeboreshwa kwa teknolojia ya kisasa kwa kutumia matundu madogo na kupunguza rufaa za kwenda nje ya nchi kwa asilimia 99.
Aidha katika kipindi hicho, huduma za kibingwa na ubingwa bobezi zimeongezeka kutoka huduma katika maeneo saba hadi 16 ya ubobezi tangu Serikali ya Awamu ya Sita iingie madarakani mwaka 2021.