TSH BIL 429.1 ZA BANDARI YA TANGA ZAANZA KUJIBU

 

TSH BIL 429.1 ZA  BANDARI YA TANGA ZAANZA KUJIBU

TSH BIL 429.1 ZA  BANDARI YA TANGA ZAANZA KUJIBU

TANGA
Kiasi cha shilingi bilioni 429.1 kilichotolewa na serikali ya awamu ya sita kwa ajili ya kufanya maboresho  katika bandari ya Tanga kimeanza kuleta faida, hii ni baada ya Bandari hiyo kupokea meli kubwa ya Makasha MV Contship yenye uwezo wa kubeba Makasha zaidi ya 1000. 
Hii ni mara ya kwanza katika historia bandari hiyo kupokea Meli yenye urefu wa mita 150 na kina cha mita 8.5 mali ya Kampuni ya MAERSK ambapo  imeweza kufunga gatini bila changamoto yoyote
KUMBUKA:- Bandari ya Tanga kabla ya maboresho, kwa mwaka ilikuwa na uwezo wa kuhudumia tani 750,000 lakini baada ya maboresho bandari ya Tanga itahudumia hadi tani 3,000,000 kwa mwaka