THAMANI YA MAUZO SOKO LA ULAYA YAFIKIA TSH TRIL 3
DODOMA
Mwaka 2023, thamani ya mauzo ya bidhaa kwenda katika Soko la Ulaya iliongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 3.836 kutoka shilingi trilioni 2.446 mwaka 2022, sawa na ongezeko la 56.8%.
Ongezeko hilo limechangiwa na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa za kilimo na viwandani kwenda katika nchi hizo.
Aidha, uagizaji wa bidhaa kutoka Jumuiya ya Ulaya ulipungua kwa 8.1% hadi shilingi trilioni 4.045 mwaka 2023 ikilinganishwa na shilingi trilioni 4.404 kwa mwaka 2022.
Upungufu huo ulitokana na kupungua kwa mahitaji ya bidhaa za viwandani na mitaji kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa zilizokuwa zinaagizwa kutoka Soko la Ulaya ikiwemo vilainishi vya magari
