DKT SAMIA KUZINDUA MRADI WA MAJI SAME-MWANGA-KOROGWE
KILIMANJARO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua mradi mkubwa wa maji Same-Mwanga-Korogwe Machi 9, 2025.
Mradi huo unatumia zaidi ya shilingi bilioni 300 ambao utanufaisha wananchi kutoka Katika wilaya za Same na Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
Aidha,mradi huo chanzo chake ni bwawa la nyumba ya Mungu na kimetengenezwa kidakio kinachochukua kutoka bwawani na kusambazwa kwenye mtambo wa kusafisha na kutibu maji wenye uwezo wa kusafisha Lita milioni kwa siku