TANZANIA ,CANADA KUSHIRIKIANA KWENYE MADINI
CANADA
Tanzania na Canada zimekubaliana kuboresha uhusiano baina ya nchi hizo mbili hasa katika eneo la kuwajengea uwezo wataalamu na wachimbaji wa madini Tanzania katika matumizi ya teknolojia ya kisasa ya uchimbaji na uchenjuaji madini. Hii ni kwa mujibu wa wizara ya madini ya Tanzania na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada, Ahmed Hussein kupitia mazungumzo yaliyofanyika Toronto, Canada.
Akitoa maelezo ya awali, Waziri Ahmed Hussein ameipongeza Tanzania kwa namna imeweka mazingira mazuri ya ukuaji wa Sekta ya Madini na kwamba Canada itaendelea kuimarisha uhusiano wake na Tanzania hasa katika eneo la kuwajengea uwezo wataalamu na wachimbaji madini kwenye matumizi sahihi ya teknolojia ya uchimbaji na uchenjuaji madini.
“Tumekuwa na miradi ya maendeleo ya elimu nchini Tamzania, hivyo kupitia vyuo vya mafunzo ya Ufundi itakuwa rahisi kuja na mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wananchi wa Tanzania, hasa wakina mama na vijana, kushiriki kikamilifu kwenye mnyororo mzima wa sekta ya madini, “amesema Hussein.