ZIARA YA BIMKUBWA DKT SAMIA MKOANI TANGA FEBRUARI 23 HADI MACHI 2, 2025

 

ZIARA YA BIMKUBWA  DKT SAMIA MKOANI TANGA FEBRUARI 23 HADI MACHI 2, 2025

ZIARA YA BIMKUBWA  DKT SAMIA MKOANI TANGA FEBRUARI 23 HADI MACHI 2, 2025

FEBRUARI 27
Uzinduzi wa miradi ya usambazaji wa Nishati safi ya kupikia (LPG) na kuzungumza na Wananchi wa Wilaya ya Muheza.
Kufungua Kiwanda cha Chokaa na Saruji (Phase two) na Kuzungumza na Wafanyakazi:- Kiwanda cha cha saruji cha Huaxin Maweni Limestone  hiki kipo eneo la Kange Industrial Area, Tanga na kina uwezo wa kuzalisha tani 750,000 za saruji kwa mwaka, uwekezaji huu ni sehemu ya utekelezaji wa mpango kazi wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ambapo China iliahidi kushawishi Makampuni yake yawekeze Barani Afrika. Kampuni ya Huaxin ni mojawapo ya Makampuni makubwa yanayozalisha saruji nchini China.
Kuweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji Tanga – Horohoro:-  Mradi huu  umegharamu kiasi cha shilingi bilioni 35.8, una jumla ya  Vituo 60 vya kuchotea maji ,unanufaisha wananchi 74,795 wa Mji wa Horohoro  na vijiji 37 vya Wilaya ya Mkinga.
Mkutano wa Hadhara:- Mhe.Rais Dkt Suluhu atafanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Handeni.
Tupo Tanga, hamna mtu atakosa kitu.