WATALII 149 WATUA KILWA

 

WATALII 149 WATUA KILWA

WATALII 149 WATUA KILWA

LINDI
Jumla ya watalii 149 wametua nchini  tarehe 15 februari katika wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi ambao wameshushwa na meli ya kifahari ya kitalii (Le Bougainville) hii ni meli ya sita kushusha watalii katika wilaya ya kilwa katika kipindi cha kuanzia Januari - Februari, 2025.
Watalii hao wametokea Mataifa ya  Marekani, Uingereza, Ubelgiji, Austalia, Ireland, Seychelles, Ujerumani na Ufaransa huku wengine wakitokea Mataifa ya Ujerumani, Israeli, Ureno na Canada
Aidha ujio wa meli hizi za watalii wa kigeni kutoka Mataifa mbalimbali ni uthibitisho tosha kuwa Tanzania inazidi kuwa  kivutio cha Kimataifa  na kuwa miongoni mwa maeneo muhimu kwa Sekta ya utalii ulimwenguni.
Sambamba na hilo, ujio wa meli hizi pia unaendelea  kudhihirisha juhudi kubwa za  kutangaza vivutio vya utalii vya nchi yetu zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya Tanzania The Royal Tour na Amaizing Tanzania.