MH.RAIS DKT SAMIA AKUTANA NA W/MKUU WA ETHIOPIA
ETHIOPIA
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Leo Februari 15 amekutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Abiy Ahmed kando ya Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
Mhe Dkt Samia yupo nchini Ethiopia tangu Februari 14 ambapo Leo Februari 15 ameshiriki Mkutano wa kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).
Vilevile mkutano huo umejadili taarifa ya ushiriki wa umoja wa Afrika kwenye mkutano wa nchi Tajiri Duniani (G20), Utekelezaji wa agenda ya 2063 ya umoja wa Afrika na taarifa kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi.
Mbali na hayo mkutano pia utajadii ajenda kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia iliyopendekezwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania..