TZ NA KOREA KUSHIRIKIANA KWENYE MADINI
DAR ES SALAAM
Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na Jamhuri ya Korea katika kutekeleza mkakati wake wa kuendeleza madini mkakati na muhimu nchini.
Hayo yamesemwa na wizara ya madini ilipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Korea nchini Tanzania, Mh.Eunju Ahn katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
"Mh.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alitupa maelekezo mahsusi ya kuhakikisha rasilimali hii ya madini mkakati tunaiwekea mfumo thabiti ili Nchi yetu ipate manufaa zaidi.
"Mojawapo ya nguzo mbili muhimu katika Mkakati huo ni kufanya utafiti wa kina ili kutambua aina na kiasi cha madini mkakati kilichopo, pamoja na kuweka mazingira rafiki ya ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani madini hayo hapa nchini,ilisema taarifa ya wizara ya madini ya Tanzania.
Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Ahn ameeleza lengo hasa ni kujitambulisha kutokana na mahusiano ya siku nyingi ya Korea na Tanzania, hususani katika sekta ya madini, na kusisitiza kwamba yupo tayari kuhakikisha mashirikiano hayo yanakuwa na tija kwa nchi zote mbili katika kuendeleza sekta ya madini hususan madini mkakati na kwakuwa tayari kampuni ya POSCO kutoka Korea imeonesha utayari wa kushiriki kwenye mradi wa madini kinywe wa Mahenge,Mkoani Morogoro