UJENZI WA BWAWA LA KIDUNDA WAFIKIA 27%

 

UJENZI WA BWAWA LA KIDUNDA WAFIKIA 27%

UJENZI WA BWAWA LA KIDUNDA WAFIKIA 27%

MOROGORO

Utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bwawa la Kidunda umefikia asilimia 27 huku kiasi cha shilingi bilioni 336 kikitarajiwa kutumika hadi kukamilika kwa mradi huo unaojengwa mkoani Morogoro  na bwawa hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji yatakayotumika kwa miaka mitatu mfululizo.
Bwawa hilo linajengwa ili kuimarisha upatikanaji wa maji hasa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, kupunguza mafuriko, na kuboresha uvuvi na kilimo miongoni mwa manufaa mengine.
Aidha Mradi huo unajumuisha ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa megawati 20 na laini ya kusambaza umeme ya kilovolti 132. Pia utahusisha ujenzi wa barabara ya changarawe yenye urefu wa kilomita 75.