KG 34,826.75 ZA DHAHABU ZALETA TSH BIL 400.22

 

KG 34,826.75 ZA DHAHABU  ZALETA TSH BIL 400.22

KG 34,826.75 ZA DHAHABU  ZALETA TSH BIL 400.22 

TANZANIA
Mwenendo wa ukusanyaji wa mrabaha kwa upande wa madini ya dhahabu umeendelea kuimarika ambapo kuanzia Julai 1, 2024 hadi Desemba 31, 2024, Serikali iliingiza shilingi bilioni 400.22 kutokana na mauzo ya kilogramu 34,826.75 za dhahabu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.55 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2023, ambapo kilogramu 32,995.54 ziliuzwa na Serikali kupata shilingi bilioni 278.86.
Katika hatua nyingine, Serikali itajenga Kiwanda cha Kusafisha Makinikia cha Tembo Nickel Refining Limited, Kahama, mkoani Shinyanga katika eneo ambalo awali lilikuwa likitumiwa na Mgodi wa Buzwagi, ambao umesitisha shughuli za uzalishaji wa dhahabu.
Mradi wa Kiwanda hicho ni moja ya miradi machache barani Afrika inayozalisha bidhaa iliyo tayari kwa matumizi, hivyo unatarajiwa kuleta tija kubwa kwa uchumi wa nchi, sambamba na kuimarisha Mchango wa Sekta ya Madini