SERIKALI YAGAWA MASHINE 185 ZA KUPIMA VIMELEA VYA KIFUA KIKUU
TANZANIA
Serikali imegawa mashine 185 za upimaji wa vimelea vya Kifua Kikuu zitakazosambazwa nchi nzima na kuzindua mpango wa kutafuta wagonjwa wa Kifua Kikuu katika halmashauri 76 za mikoa tisa (9) huku lengo likiwa ni kusambaza mashine hizo katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na mikoa miwili upande wa Zanzibar.
Uwekezaji huu unatarajiwa kupanua mtandao wa upimaji wa Kifua Kikuu nchini kwa kusogeza huduma karibu na wananchi ili kumwezesha kila mwananchi anayegundulika kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu kuanza matibabu kwa wakati ili asiendelee kuambukiza watu wengine.
Tunapatikana Instagram,Facebook,X, TikTok, YouTube:-BimkubwaTanzania