MCHUCHUMA NA LIGANGA KUTEKELEZWA 2025/26

 

MCHUCHUMA NA LIGANGA KUTEKELEZWA 202526

MCHUCHUMA NA LIGANGA KUTEKELEZWA 2025/26

NJOMBE
Serikali katika mwaka wa fedha 2025/26 itaanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga ambao utatekelezwa na Kampuni ya Shudao Group yenye makao yake makuu nchini China.
Kuanzia mwezi huu(Februari), kampuni itakamilisha taratibu zake za kuhamisha hisa, mchakato ambao utachukua takriban miezi mitatu kabla ya kutekelezwa kwa mradi huo
Aidha Hifadhi ya madini ya Liganga inafikia tani milioni 129 huku Mchuchuma ikiwa na akiba ya tani milioni 422 za makaa ya mawe.
Eneo la Mradi wa Mchuchuma lina ukubwa wa kilometa za mraba 141 na Kiwanja cha Chuma cha Liganga kina ukubwa wa Kilomita za Mraba 179.
Mbali na madini ya chuma na makaa ya mawe, mgodi wa Liganga una madini mengi ya Vanadium Pentoxide, Titanium, Ammonium Sulphate na Sulphur.
Mradi wa Liganga unatarajiwa kuwa mradi wa pili kwa ukubwa wa chuma hadi chuma barani Afrika baada ya ule wa Afrika Kusini.