TSH BIL 521 ZAKUSANYWA KWENYE MADINI
DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Madini imekusanya shilingi bilioni 521 katika kipindi cha Julai 1, 2024, hadi Desemba 31, 2024. Hii ni sawa na asilimia 52.2 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 1 kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Mafanikio hayo yanatokana na usimamizi mzuri, udhibiti madhubuti, na weledi katika ukusanyaji wa mapato kwenye sekta ya madini ambapo wizara imepiga hatua kubwa ikilinganishwa na mwaka wa fedha wa 2015/16 ambapo ilikusanya shilingi bilioni 161 kwa mwaka mzima na mwaka huu ndani ya nusu ya kwanza tayari tumekusanya asilimia 52.2 ya lengo la Shilingi trilioni 1 kwa Mwaka wa Fedha wa 2024/25.
Katika hatua nyingine, leseni kubwa na za kati za madini ambazo hazijaendelezwa zitarudishwa Serikalini zitakabidhiwa kwa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) kwa ajili ya kuziendeleza kwa manufaa ya taifa.