KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA DKT SAMIA
DODOMA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imempongeza Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya kuhakikisha makundi mbalimbali ikiwamo vijana na watu wenye ulemavu yanajikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.
Akizungumza Mwishoni mwezi Januari 2025 katika kikao cha kamati jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq amesema wameona jitihada hizo za Mhe. Rais kupitia utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na programu ya ukuzaji ujuzi kwa vijana zinasaidia wananchi kufikia malengo.
Mhe. Toufiq amepongeza jitihada za serikali za kuwawezesha vijana kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Vijana na kuwashauri wadau wengine ikiwamo kampuni kubwa nchini zishirikishwe kuchangia kutunisha mfuko huo ili vijana wengi wanufaike