TANZANIA NA QATAR KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA YA KAZI NA AJIRA

TANZANIA NA QATAR KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA YA KAZI NA AJIRA

TANZANIA NA QATAR KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA YA KAZI NA AJIRA

SAUDI ARABIA
Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kazi wa Qatar Dkt. Ali Bin Saeed Bin Samikh kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika masuala ya sekta ya kazi na ajira ili kuwezesha Watanzania kunufaika na fursa za ajira nchini Qatar .
Makubaliano kutoka wizara hizo mbili yamefanyika Januari 29, 2025 Riyadh nchini Saudi Arabia ambapo wameelekeza timu ya Wataalam inayohusisha pande zote kukutana haraka kutathmini utekelezaji wa hati ya makubaliano kati ya Tanzania na Qatar iliyosainiwa mwaka 2014 nchini Qatar.