TANZANIA NA KOREA KUBORESHA MAABARA YA KITAIFA (AFYA)
DODOMA
Serikai ya Tanzania na Korea zimeazimia kuendelea kuboresha Maabara ya Kitaifa ya Afya ya Umma kwa ajili ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza, kuimarisha usimamizi wa hospitali, pamoja na ukarabati na ujenzi wa wodi maalum za watoto wachanga wagonjwa (NICU).
Hatua hii ni muendelezo wa ushirikiano uliopo baina ya Serikali Tanzania na Jamhuri ya Watu wa Korea uliochangia kuimarika kwa huduma za afya nchini katika nyanja za miundombinu ya vituo vya afya, vifaa tiba na mafunzo mbalimbali kwa watoa huduma za afya.
Aidha katika kipindi cha miaka mitano (5), Serikali ya Tanzania imenufaika na ushirikiano uliopo kati yake na Korea kupitia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Nne wa Sekta ya Afya (HSSP-IV) pamoja na Mpango Mkakati wa Tano (5) kupitia Shirika la Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH).