RWANDA YAIPONGEZA TANZANIA UWEKEZAJI BANDARI YA DAR

 

RWANDA YAIPONGEZA TANZANIA UWEKEZAJI BANDARI YA DAR

RWANDA YAIPONGEZA TANZANIA UWEKEZAJI BANDARI YA DAR 

TANZANIA
Mamlaka ya Forodha nchini Rwanda (RRA) imeipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) chini ya usimamizi wa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji na uboreshaji mkubwa uliyofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam kuhudumia meli na shehena kwa ufanisi.
Pongezi hizo zimetolewa na Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo Ronald Niwenshuti alipouongoza ujumbe wake kutembelea Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni, kwa lengo la kuona namna bandari hiyo inavyohudumia shehena na maboresho ya miundombinu yalivyofanyika.
Akitoa salamu za Wafanyabiashara wa nchini Rwanda amesema kuwa wameridhishwa na kasi ya Bandari ya Dar es Salaam katika kuhudumia shehena kwa kuwa mizigo yao inawafikia kwa haraka tofauti na awali.
Aidha,Rwanda ni nchi ya tatu Kati ya nchi zinazoingiza shehena kwa kiwango cha juu zaidi kupitia Bandari ya Dar es Salamm ikiongozwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia.