BARABARA MASUMBWE - IGOMBE RIVER YAPANDA HADHI

BARABARA MASUMBWE - IGOMBE RIVER YAPANDA HADHI

BARABARA MASUMBWE - IGOMBE RIVER YAPANDA HADHI

SHINYANGA
Serikali kupitia   Wizara ya Ujenzi imeipandisha hadhi barabara ya Masumbwe - Mwambomba- Bugomba A - Igombe River (Km 124) kutoka Wilaya na kuwa ya Mkoa ili iweze kuhudumiwa na TANROADS na hivyo kufanya fedha za matengenezo ya barabara katika Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga  kuongezeka kutoka Bilioni 1.5 kwa mwaka wa fedha 2023/24 hadi kufikia Bilioni 2.7 kwa mwaka wa fedha 2024/25.