DKT SAMIA APOKEA TUZO YA THE GLOBAL GOALKEEPER
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Leo Februari 4,2025 amepokea Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award kutoka kwa Rais wa Kitengo cha Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Gates, Dkt. Anita.
Tuzo hiyo hutolewa kwa viongozi waliowezesha nchi zao kuharakisha maendeleo kuelekea kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Mhe. Rais Samia amepewa Tuzo hiyo katika kipengele cha mapambano dhidi ya vifo vya wamamawajawazito na watoto wachanga chini ya umri wa miaka mitano.
Aidha tuzo hiyo imetolewa kwa mara ya kwanza nje Ya Marekani(hapa nchini Tanzania)na Mhe Rais Samia ndiye Rais wa kwanza kutoka nchi za Afrika kutunukiwa.