TSH BIL 4.6 KUJENGA DARAJA LA TANGANYETI
ARUSHA
Serikali kupitia wizara ya ujenzi imemkabidhi kazi ya ujenzi wa daraja la Tanganyeti wilayani Longido lenye urefu wa mita 40 katika barabara ya Arusha-Namanga Mkandarasi Jiangx Geo Engineering huku shilingi bilioni 4.6 zikitumika katika ujenzi huo.
Daraja la Tanganyeti likikamilika litakuwa na uwezo wa kupitisha uzito wa tani 80 na ujenzi wake utatumia siku 365
Barabara ya Arusha - Namanga inaunganisha Tanzania na Kenya na ni barabara ya utalii hivyo ujenzi wake utaleta tija kwa wananchi na watumiaji wa barabara hiyo.