TSH TRIL 2.9 ZABORESHA NA KUENDELEZA MIRADI YA TACTIC
TANZANIA
Jumla ya miradi yenye thamani ya Shilingi Trilioni 2.9 sawa na Dola za Marekani Bilioni 1.108 inatekelezwa maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni adhma ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kupitia Miradi ya uendelezaji wa miji 45 Tanzania (TACTIC) ili kuhakikisha utoaji bora wa huduma kwa wananchi nchini Tanzania.
Miradi hiyo inasimamiwa na OR-TAMSMI na kutekekezwa na TARURA kupitia kikundi kazi cha uratibu wa miradi “projects coordiination team (PCT) ambayo ni mradi wa Uboreshaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP2) na uendelezaji wa bonde la Mto Msimbazi Mkoani Dar es Salaam pamoja na mradi wa TACTIC unaotekelezwa kwenye miji 45 nchi nzima.
Lengo la miradi hiyo ni kuboresha na kuendeleza huduma za usafiri na usafirishaji pamoja na huduma mbalimbali za kijamii.
