TSH BIL216 + ZAIMARISHA HAKI
TANZANIA
Kiasi cha dolla za Marekani milioni 91 (zaidi ya shilingi bilioni 216 ) mkopo kutoka Benki ya Dunia zimetumika kuboresha mfumo wa utoaji haki ikiwemo ujenzi wa Vituo Vipya tisa vya Haki Jumuishi nchini.
Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania zilipitisha Awamu ya Pili ya Mpango wa Maboresho baada ya Majengo Jumuishi sita yaliyozinduliwa na Mhe Rais Dkt Samia tarehe 6 Oktoba, 2021 na kuonesha mafanikio makubwa katika kutoa haki.
Hivi sasa serikali inajenga Vituo Jumuishi Simiyu, Geita, Katavi, Njombe, Songwe, Songea, Lindi, Singida na Pemba.
