TSH BIL 18.05 KUJENGA MADARAJA USHETU

 

TSH BIL 18.05 KUJENGA MADARAJA USHETU

TSH BIL 18.05 KUJENGA MADARAJA USHETU

SHINYANGA
Serikali itatumia kiasi cha shilingi bilioni 18.05 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja makubwa manne ya Ubagwe, Kasenga, Ng’hwande na Mwabomba yaliyoathiriwa na mvua za El Nino katika Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga na Ujenzi huo utatekelezwa na wakandarasi wazawa kutoka Kampuni ya Salum Motors na Jonta Investment ambao wamekabidhiwa kazi Novemba 30, 2024.
Ujenzi wa Daraja la Ubagwe (m 40) unagharimu Bilioni 4.14, Daraja la Kasenga (m 60) unagharimu bilioni 5.13, Daraja la Ng’hwande (m 40) unagharimu billion 4.28 na Daraja la  Mwabomba (m 50) unagharimu bilioni 4.5 pamoja na ujenzi wa tuta la barabara (m 300) kwa kiwango cha changarawe katika kila daraja kwa muda wa mwaka mmoja (miezi 12).
Ujenzi wa madaraja hayo ukikamilika utaondoa changamoto na adha ya wananchi waliyokuwa wakiipata ya kukatika kwa mawasiliano ya barabara misimu ya mvua kila mara.