RIPOTI - SERIKALI IMEWEKA MKAZO ONGEZEKO MAZAO YA BAHARI
TANZANIA
Taarifa ya hali ya uchumi ya mwaka 2023 na mpango wa maendeleo wa taifa wa 2024/25 zimebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo wa kipekee na kuongeza nguvu katika kuongeza pato la mazao ya baharini katika kipindi uongozi wake.
Dkt Samia Suluhu Hassan amewezesha ongezeko kubwa la idadi ya samaki katika maji ya Tanzania na pia amekuza ufugaji wa kisasa wa samaki miongoni mwa wawekezaji mbalimbali kupitia sera rafiki zinazotambua sekta ya uvuvi kama nyenzo muhimu ya kukuza uwezo wa kiuchumi wa nchi.
Sehemu ya juhudi zinazofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni pamoja na kupambana na uvuvi haramu kwa kutunga sheria kali za kulinda mazao ya baharini na kufadhili kwa kiasi kikubwa doria ili kudhibiti uvuvi haramu.
Aidha, kwa kutambua umuhimu wa mauzo ya samaki nje ya nchi, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuweka mikakati ya kisasa ya kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha samaki kwa bei nafuu nchini, hivyo kuhamasisha wafugaji wengi zaidi kushiriki.
Ni wazi kuwa umaarufu wa Tanzania katika soko la kimataifa umekuwa ukirejea kwa kasi kutokana na bidhaa bora za samaki zinazotoka nchini humo.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewezesha uanzishaji wa skimu za kisasa zinazotumika kwa ufugaji wa samaki kwenye maboma ya kitaalamu, ambazo zimebainika kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la tani zilizotajwa kwenye ripoti hiyo.
Ripoti ya mwaka 2019/20 ilirekodi uzalishaji wa samaki wa tani 497,567.28, wakati kipindi cha 2023/24 kilishuhudia ongezeko kubwa la uzalishaji kufikia tani 513,218.90.
Azma ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kutimiza ndoto za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kwa kuifanya Tanzania kuwa kinara katika uzalishaji wa samaki barani Afrika.
