TSH BIL 18 ZANUNUA VIFAA VYA TEHAMA ELIMU SEKONDARI

 

TSH BIL 18 ZANUNUA VIFAA VYA TEHAMA ELIMU SEKONDARI

TSH BIL 18 ZANUNUA VIFAA VYA TEHAMA ELIMU SEKONDARI

DAR ES SALAAM
Serikali kwa kutambua umuhimu wa matumizi ya TEHAMA katika ujifunzaji na kujenga umahiri uliokusudiwa kwenye Mitaala kwa wanafunzi wa Sekondari, katika kipindi cha mwaka 2023/2024 imetoa jumla ya Shilingi Bilioni 18 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya TEHAMA, ambapo kupitia Programu ya SEQUIP, Shule za Sekondari 1,500 zinatarajiwa kunufaika.
Vifaa hivyo vinalenga kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji kwa njia ya kisasa kwa kutumia na kujifunza TEHAMA ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia Duniani.
Katika kufanikisha azima hii, Serikali imetoa mafunzo ya matumizi ya TEHAMA na huduma ndongondogo ya vifaa hivyo kwa walimu 3,132 wa Shule za Sekondari ambapo utoaji wa mafunzo kwa walimu hao umelenga kuhakikisha walimu wamejengewa uwezo katika kutunza Vifaa vilivyonunuliwa, kutumia vifaa kwa ufasaha ikiwemo kuwaelekeza wanafunzi na kufanya huduma ndogondogo inapotokea hitilafu katika vifaa husika.
Aidha manunuzi ya vifaa vya TEHAMA yamezingatia mwongozo wa SEQUIP ( ICT package) kwa kila Shule ya Sekondari inayonufaika. Kufuatia mwongozo huo vifaa vilivyonunuliwa ni  Kompyuta za mezani 1,848, UPS 462, Kompyuta Mpakato 231, Projekta 231 na Projekta “screen” 231.