TSH BIL 972 KUONGEZA VYUO 14 MWAKA UJAO

 

TSH BIL 972 KUONGEZA VYUO 14 MWAKA UJAO

TSH BIL 972 KUONGEZA VYUO 14 MWAKA UJAO

MWANZA
Kiasi cha shilingi bilioni 972 kimetolewa na serikali ya awamu ya sita chini a Mhe Rais Dkt Suluhu Hassan kwa ajili ya kujenga vyuo vya elimu ya juu vinavyojengwa katika mikoa 14 ambavyo vinatarajiwa kufanya kazi katika mwaka ujao wa masomo (Hii ni kulingana na Naibu Waziri wa Elimu, Bw Omary Kipanga).
Kufutia mradi huo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinasimamia ujenzi wa kampasi katika mikoa ya Kagera na Lindi, wakati Chuo Kikuu cha Ardhi kinashughulikia kampasi ya Mwanza na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kinaendelea na kampasi ya Kigoma.
Aidha,Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Mwalimu Julius Nyerere kinajenga kampasi mkoani Tabora,Taasisi ya Uhasibu Arusha inaendeleza kampasi mkoani Ruvuma na Taasisi ya Uhasibu Tanzania inajenga moja mkoani Singida.
Takribani asilimia 70 ya fedha za mradi zitatumika kwa ajili ya miundombinu,ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kumbi za mihadhara, maabara,majengo ya utawala na kumbi za mikutano.
Fedha hizo pia zitagharamia ununuzi wa vifaa vya TEHAMA ili kuvifanya vyuo hivyo vipya kuwa vya kisasa, hivyo kuwawezesha wanafunzi wa Kitanzania kuhudhuria mihadhara ya mtandaoni kutoka vyuo vikuu duniani kote.
Sambamba na hilo, serikali inaimarisha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa kuanzisha vyuo vipya nchi nzima.
Songwe ndio mkoa pekee ambao awali haukuwa na chuo cha VETA,lakini ujenzi unaendelea na serikali imejipanga kuhakikisha kila wilaya inakuwa na chuo cha VETA, huku ujenzi ukiendelea katika wilaya 64 zilizobaki.