TSH BIL 40.7 ZATEKELEZA MIRADI 108 (TANAPA)

 

TSH BIL 40.7 ZATEKELEZA MIRADI 108 (TANAPA)

TSH BIL 40.7 ZATEKELEZA MIRADI 108 (TANAPA)

TANZANIA
Kiasi cha shilingi bilioni 40.7  kinatumika kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya kutekeleza miradi 108 ya ujirani mwema katika sekta za elimu, afya, usalama, maji na barabara.
Katika fedha hizo, kiasi cha  Shilingi bilioni 36.5  ni kupitia ufadhili wa mradi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) na Shilingi bilioni 4.2 kupitia fedha za Miradi ya Maendeleo.
Kati ya miradi hiyo, miradi 75 imekamilika, miradi 10 iko katika hatua za ukamilishaji na miradi 23 ipo katika hatua ya awali ya utekelezaji. 
Aidha, miradi iliyokamilika ni pamoja na ujenzi wa vyumba 44 vya madarasa na ofisi 16 za walimu katika Wilaya za Serengeti, Ngorongoro, Bariadi, na Bunda; mabweni 4 ya wasichana katika shule za sekondari na msingi zilizopo Wilaya za Mpanda, Same, Mwanga na Serengeti; na nyumba 15 zenye uwezo wa kukaa familia 30 za walimu katika Wilaya za Serengeti 9 na Ngorongoro 6.