MRADI WA REGROW WAINUA HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI
MOROGORO.
Hifadhi ya Taifa ya Mikumi imepata mafanikio makubwa yanayotokana na utekelezaji wa mradi wa Usimamizi wa Maliasili Endelevu kwa Utalii na Ukuaji (REGROW) ambao umeleta mabadiliko ya kihistoria katika sekta ya utalii na uhifadhi ndani ya ukanda wa uhifadhi wa Kusini mwa Tanzania.
Mradi huo umeanzisha miundombinu mbalimbali ya kisasa ndani ya hifadhi hiyo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kiwanja cha ndege.Maboresho haya yamesaidia kuongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya watalii ambapo hapo awali mikumi ilikuwa inapokea ndege 13 kwa siku na sasa hivi wanapokea ndege 30 zinazobeba abiria kati ya 35 hadi 40 kwa siku.
ZINGATIA:-Mradi wa REGROW,ambao ni mpango wa serikali unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa bajeti ya jumla ya dola za Marekani milioni 150 (takriban bilioni 345),unalenga kuimarisha usimamizi wa maliasili na mali za utalii kusini mwa Tanzania huku ukitoa fursa mbadala za kujikimu kimaisha kwa wazawa.
