TSH BIL 108 ZAINGIZA DARASANI WASICHANA 4,843
TANZANIA
Kiasi cha shilingi bilioni 108 kilichotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha uongozi wake kimeboresha miundombinu ya elimu nchini na kufanikisha kuingiza darasani kwenye Shule za Wasichana za Sayansi za Mikoa ambazo zimejengwa kwenye mikoa yote 26 ya Tanzania Bara Jumla ya wanafunzi wa kike 4,843.
Katika wanafunzi hao wa kike, kidato cha kwanza wanafunzi waliopo ni 1,596, Kidato cha Pili (139), Kidato cha Tano (2,355) pamoja na Kidato cha Sita ni 753.
Katika fedha hizo, mikoa yote imepata Sh. Bilioni 4.1 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu yote muhimu ya shule na baadhi kuongezewa Sh.Milioni 350 kwa ajili ya ukamilishaji wa bwalo.
