RIPOTI-HAKI ZA BINADAMU,UTAWALA BORA VYAIINUA TANZANIA

 

RIPOTI-HAKI ZA BINADAMU,UTAWALA BORA VYAIINUA TANZANIA

RIPOTI-HAKI ZA BINADAMU,UTAWALA BORA VYAIINUA TANZANIA

DAR ES SALAAM 
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema,Tanzania inapiga hatua kubwa katika kusimamia haki za binadamu na utawala bora, inayoonesha mwelekeo mzuri katika kuhakikisha wananchi wake wanapata haki zao za msingi.
Jaji mstaafu Mathew Mwaimu amesema hayo wakati wa kufunga maadhimisho ya siku tatu ya Siku ya Haki za Binadamu yaliyofanyika kuanzia Desemba 12 hadi  14, 2024 kwenye Viwanja vya Mwembeyanga Temeke,Dar es Salaam.
"Nchini Tanzania, tunapiga hatua kubwa katika haki za binadamu.Pamoja na changamoto tunazokabiliana nazo, nchi inafanya vizuri, ikionesha mabadiliko chanya ya serikali katika kuhakikisha Watanzania wanapata haki zao za msingi kikamilifu,”alisema Jaji Mwaimu.
Alisisitiza,juhudi kubwa zimeifanya Tanzania kuwa kinara katika uzingatiaji wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kuboreshwa kwa uhuru wa vyombo vya habari ikilinganishwa na nchi nyingine jirani.
Jaji Mwaimu amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake makini katika kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari, huku akisisitiza agizo lake kwa taasisi na wizara zote za serikali kujumuisha vitengo vya mawasiliano na kuhakikisha wananchi wanapata habari.
"Rais Samia alikubali mapendekezo yote na kuibadilisha tume kuwa kamati ya utekelezaji,"alisema na kuongeza kuwa hatua hiyo imesababisha utekelezaji wa mipango kadhaa, ikiwa ni pamoja na maagizo kwa taasisi na wizara husika kufanya mageuzi katika sekta ya haki jinai.