MAFANIKIO TELE HUDUMA ZA AFYA SHINYANGA

 

MAFANIKIO TELE HUDUMA ZA AFYA SHINYANGA

MAFANIKIO TELE HUDUMA ZA AFYA SHINYANGA

SHINYANGA
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeboresha kwa kiasi kikubwa huduma za afya Shinyanga Mjini kwa kukamilisha ujenzi wa Zahanati na vituo vya Afya ambavyo ujenzi wake ulisimama kabla ya kuingia kwake madarakani.
Vituo vya Afya na Zahanati mpya zaidi ya tatu zimejengwa na kukamilika na sasa kuna uhakika mkubwa wa kupata huduma bora za afya.
Katika kipindi cha uongozi wake, Rais Dkt. Samia ameendelea kutoa fedha za miradi iliyokuwa imekwama, ambapo amefanikiwa kujenga vituo vya Afya kwa thamani ya shilingi milioni 500, kituo cha Afya Lubaga (104,000,000), miradi hii imekamilika na inatoa huduma kwa wananchi.
Sambamba na hilo ipo miradi minginne ambayo ilikwama kwa muda mrefu ni Zahanati ya Bushola iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 56, Zahanati ya Masekelo Tshs (70,000,000), Zahanati ya Songambele (Kitangili) Tshs (60,000,000) na Zahanati ya Seseko Tshs (85,000,000).
Vilevile katika kituo cha Afya kambarage amefanikiwa kukarabati wodi na jengo la OPD kwa Tshs (500,000,000). 
Aidha hadi kufikia 2024/2025 zahanati ambazo zipo kwenye ukamilishaji ni pamoja na zahanati ya Mwamagunguli (kolandoto), Zahanati ya Mwagala (Ibadakuli) na Zahanati ya Ibinzamata (Ibinzamata)
MUHIMU:- serikali imefanikiwa kufanya ukarabati katika Hospitali ya manispaa ya Shinyanga kwa kutumia zaidi ya shilingi 1.3 billioni.