TANZANIA, EU KUSHIRIKIANA UTAFITI WA KINA WA MADINI
SERIKALI imeahidi kuendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) katika kufanya utafiti wa kina utakaosaidia kupata taarifa sahihi za maeneo madini yanapopatikana ili kuongeza uwekezaji katika uvunaji rasilimali madini hususani madini mkakati kwa manufaa na maslahi ya Watanzania.
(Taarifa hii ni kwa mujibu wa wizara ya madini ilipokutana na ujumbe wa uwakilishi kutoka EU ukiongozwa na Mkurugenzi wa Miradi ya EU Bara la Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, Hanspaul Stausboll)
Mazungumzo hayo na ujumbe wa EU yamejikita katika kuimarisha mashirikiano kwenye uendelezaji sekta ya madini huku ikichagizwa na ukweli kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache ulimwenguni zilizobarikiwa madini mbalimbali yakiwemo ya kimkakati kama graphite ambayo ni kivutio kwa wawekezaji wengi kutokana na mwelekeo wa dunia katika kupunguza hewa ukaa ifikapo 2050 kwa matumizi ya nishati safi
Eneo la pili ni kuyaongezea thamani madini ndani ya nchi badala ya kusafirisha yakiwa ghafi ambapo Nchi tunapoteza mapato, ajira na ustawi wa watanzania.
Aidha,Hadi hivi Sasa tayari Serikali imeshaanza kufanya kazi na EU katika utafiti kupitia Ubalozi wa Hispania hapa nchini.
