TZ, DRC ZASAINI MKATABA BANDARI ZA KALEMIE,MOBA
DODOMA
SERIKALI ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimetiliana saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa kuboresha Bandari ya Kimataifa ya Kalemie na Moba pamoja na ujenzi wa bandari kavu ya Kasambondo ili kufanya shughuli za bandari kuwa za kisasa na kurahisisha usafirishaji wa mizigo kati ya DRC na Tanzania.
Katika ushirikiano huo nchi hizi mbili zimekubali pia kuboresha miundombinu ya reli inayopatikana DRC
Makubaliano hayo yalitiwa saini kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na tayari mshauri wa mradi huo amekabidhiwa eneo hilo.
KUMBUKA:- Kalemie, ni mji kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ni bandari kwenye ukingo wa magharibi wa Ziwa Tanganyika ambapo Mto Lukuga unatoka.