MAAZIMIO 7  BIMA YA AFYA KWA WOTE

 

MAAZIMIO 7  BIMA YA AFYA KWA WOTE

 MAAZIMIO 7  BIMA YA AFYA KWA WOTE

ARUSHA 
Kongamano la Bima ya Afya kwa Wote na Jukwaa la Ugharamiaji wa huduma za afya limehitimishwa Novemba Mosi 2024 Mkoani Arusha( baada ya kikao cha siku nne kilichohusisha wadau wa sekta ya afya) huku wataalamu na wadau wa sekta ya afya wakikubaliana kutekeleza maazimio saba (7) yatakayosaidia utekelezaji wa ufanisi wa huduma za Bima ya Afya kwa Wote. 
1.     Azimio la kwanza ni wataalamu wa sekta kukubaliana  kutumia utaalamu wao kupata au kuongeza rasilimali fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa bima ya afya kwa wote.  
2.      kuandaa mkakati wa utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote ambao utabainisha majukumu na wajibu wa wadau wote wa sekta ya afya na hapa amesisitiza kuwa suala la bima ya afya kwa wote siyo jukumu la sekta ya afya pekee. 
3.      Wataalamu wamekubaliana pia kuhakikisha viwango vya uchangiaji kwa wanachama vinazingatia uwezo na kuwa na namna bora ya uchangiaji hususan kwa sekta isiyo rasmi
4.     Kuandaa mpango mkakati wa kutekeleza dhana ya ulazima kwa watu wote kujiunga na bima. 
5.     Kuandaa mpango shirikishi wa utoaji wa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kujiunga na bima ya afya kwa kuwashirikisha wadau wote. 
6.     kuimarisha matumizi ya mifumo ya TEHAMA ili kuwezesha utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, hususani usajili wa wanachama na vituo, uwasilishaji, uchakataji na ulipaji madai
 7.     Serikali kuendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali katika dhana nzima ya utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote.  
Kwa upande wao wadau wa sekta ya afya kwa pamoja wameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote pamoja na kutoa msaada wa kitaalamu na rasilimali katika kuanzisha vyanzo endelevu vya kugharamia huduma za afya nchini Tanzania.