UMEME KUSAMBAZWA KWENYE VITONGOJI MWEZI DESEMBA

 

UMEME KUSAMBAZWA KWENYE VITONGOJI MWEZI DESEMBA

UMEME KUSAMBAZWA KWENYE VITONGOJI MWEZI DESEMBA

TANZANIA
Serikali ina mpango wa kuzindua mradi mpya wa kusambaza umeme kwenye vitongoji Desemba 2024  ambao utahusisha ujenzi wa njia za kusambaza umeme za kati na za chini.
Mradi huo utakaoanza Desemba 2024, umefanyiwa maboresho makubwa kwani una transfoma zenye uwezo wa Kilo-volt 50, 100 na 200 (kVA), kulingana na ukubwa wa kijiji.
Aidha serikali inaendelea kusambaza umeme vijijini ikiwa ni pamoja na maeneo ya nusu mijini.
MUHIMU:- Hadi Julai, mwaka 2024 Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uliunganisha umeme jumla ya vijiji 12,031, sawa na asilimia 98 ya vijiji vyote.