MTWARA, LINDI KWENYE GRIDI YA TAIFA (UMEME)
DODOMA
Serikali inatekeleza mradi wa umeme Gridi ya Taifa kwa kuiunganisha mikoa ya Mtwara na Lindi kutokea Songea kwa kupitia njia ya Tunduru, Masasi -Mahumbika.( kwa mujibu wa wizara ya nishati Bungeni Jijini Dodoma Novemba 4, 2024).
Aidha wizara ya nishati inatekeleza agizo la Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan la kutaka kuwalipa fidia wananchi wote waliopisha mradi wa kuunganisha umeme kwenye Gridi ya Taifa kwenda mikoa ya Mtwara na Lindi.