TSH MIL 500 KUBORESHA TENKI LA MAJI MKATA
TANGA
Serikali imepanga kutumia Shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuboresha tenki la maji lililopo kata ya Mkata ili liweze kuwahudumia wananchi wa kijiji cha Manga kilichopo kata ya Mkata, Wilayani Handeni mkoani Tanga kwa kuhifadhi maji kutoka Bonde la Wami/Ruvu.
Tenki hilo lenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya lita laki tano za maji linatakiwa liwe suluhu kwa wananchi wa Manga na maeneo yote ya Mkata.
ZINGATIA:- Asilimia ya upatikanaji wa maji mijini na vijijini imeendelea kuongezeka siku baada ya siku kutokana na juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
