TSH BIL 50.1 KUIPANUA MUHAS
DAR ES SALAAM
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimetiliana saini mkataba wa ushirikiano wa shilingi bilioni 50.1 na kampuni mbili za ujenzi wa kujenga Chuo kipya cha Tiba katika kampasi yake ya Mloganzila.
Ujenzi huo utakaofanywa na kampuni ya Mohamed Builders Limited na kampuni ya Kichina ya Hainan International Limited, unajumuisha uendelezaji wa kumbi za mihadhara zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,400, jengo la utawala lenye ofisi za watumiaji 450, maktaba na jengo la TEHAMA linaloweza kubeba watumiaji 550 mara moja.
Awamu ya kwanza, yenye thamani ya 23.4bn/-, itahusisha ujenzi wa jengo la utawala, maktaba, vifaa vya TEHAMA, na miundombinu ya ziada, ikijumuisha uwanja wa mpira na njia za waenda kwa miguu.
Awamu ya pili yenye thamani ya 26.7bn/- italenga kujenga kumbi za mihadhara, maabara, hosteli za wanafunzi na mikahawa.
Mradi huu ni sehemu ya mpango wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), ni sehemu muhimu ya juhudi za serikali za kuimarisha sekta ya afya nchini Tanzania.
FAHAMU:- Uwekezaji wa Serikali katika miundombinu ya afya ni kipaumbele kilichoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama tawala cha CCM 2020-2025, Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP III) wa 2021/22-2025/26, na Dira ya Maendeleo 2025
