RUZUKU YA TSH BIL 12.7 KUINUFAISHA MUHAS

 

RUZUKU YA TSH BIL 12.7 KUINUFAISHA MUHAS

RUZUKU YA TSH BIL 12.7 KUINUFAISHA MUHAS

DAR ES SALAAM
Serikali ya Tanzania kupitia Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)  na Sweden zimesaini makubaliano ya ruzuku ya shilingi bilioni 12 .7 kwa miaka sita ili kuimarisha utafiti, uvumbuzi na mafunzo kwa wanafunzi wa Uzamivu na Shahada ya Kwanza ambapo utekelezaji wa mkataba huo utaanza rasmi Desemba 2024 na kuendelea hadi Juni 2030.
Katika ushirikiano huo, MUHAS pia inashirikiana na vyuo vikuu vitatu vya Sweden, vikiwemo Umeå, Chuo Kikuu cha Uppsala na Taasisi ya Karolinska, ambao watashiriki kama wasimamizi-wenza wa wanafunzi wa PhD.
Ushirikiano huo umelenga katika kuimarisha jukumu na uwezo wa chuo kikuu kushughulikia changamoto muhimu za kiafya za umuhimu wa kitaifa, kama vile rasilimali watu kwa afya, sera za afya na miongozo, na mabadiliko ya mazingira ya magonjwa.