TANZANIA YAONGOZA MAUZO UTALII NJE YA NCHI
DAR ES SALAAM
TANZANIA inaongoza kwa mauzo ya huduma za utalii nje ya nchi, ikichangia zaidi ya nusu ya mapato kwa mauzo ya nje ya nchi kwa ukanda wa Afrika Mashariki ikiwa na dola za Marekani bilioni 3.4 (takribani shilingi trilioni 8.97/- ) mwaka 2023 kutoka dola za Marekani bilioni 2.6 (takribani shilingi trilioni 6.86) mwaka 2019 kati ya nchi za Afrika Mashariki.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EABC, Adrian Njau, jijini Dar es Salaam Novemba 28 wakati wa warsha ya uhamasishaji wa sekta mbili ambazo ni utalii na huduma zinazohusiana na usafiri kuhusu Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) kuhusu biashara ya huduma kwa wadau wa usafiri kuwa eneo la EAC ndilo muuzaji mkuu wa huduma nje ya nchi.
Kutokana na taarifa ya Kanda nzima,(EAC) Tanzania iliuza nje huduma za usafiri zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 6.3 (trilioni 16.62) mwaka 2023 dhidi ya dola za Marekani bilioni 1.2 (trilioni 3.16) zilizoagizwa kutoka nje.
Tanzania inaongoza kwa mauzo ya nje ya nchi kwa dola za Marekani bilioni 2.4 (6.33tri/-), ambayo ni takriban asilimia 52 ya mauzo ya nje ya EAC dhidi ya dola za Marekani bilioni 1.8 (4.74tri/- za Kenya), ambayo ni asilimia 39 ya jumla EAC mauzo ya nje.
Tanzania inaweza kukuza huduma zake za usafirishaji katika nchi hizo kwa kuimarisha huduma zake za usafiri, miundombinu, bandari na kurahisisha biashara na kufanya njia zake za usafiri kuwa na ufanisi na ushindani.
