MHE RAIS SAMIA KUONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA DK NDUGULILE

MHE RAIS SAMIA KUONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA DK NDUGULILE

MHE RAIS SAMIA KUONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA DK NDUGULILE

DAR ES SALAAM
Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan atawaongoza waombolezaji katika kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa  mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) barani Afrika na Mbunge wa Kigamboni jijini Dar es Salaam  Marehemu Dk Faustine Ndugulile katika hafla ya kuaga iliyopangwa kufanyika Jumatatu Desemba 2, 2024 katika Viwanja vya Karimjee.
Dk Ndugulile aliaga dunia usiku wa Novemba 27, 2024, nchini India alipokuwa akipokea matibabu na Kwa mujibu wa ratiba ya maziko iliyotolewa na Ofisi ya Bunge, Dk Ndugulile atazikwa Desemba 3, 2024, Kigamboni, Dar es Salaam.