DKT SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA 21 WA EAMJA JIJINI ARUSHA

 

DKT SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA 21 WA EAMJA JIJINI ARUSHA

DKT SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA 21 WA EAMJA JIJINI ARUSHA

ARUSHA 
Mhe Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua Mkutano Mkuu wa 21 wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki (EAMJA), utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Jumatatu tarehe 2 hadi  7 Desemba 2024.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tukio hilo, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Dk Gerald Ndika amesema Mhe Rais Samia amepanga kufungua rasmi kongamano hilo Jumanne tarehe 3 Desemba.
Mkutano huo utawakutanisha washiriki 392 kutoka Uganda, Kenya, Burundi, Sudan Kusini, Tanzania Bara na Zanzibar.
Mkutano huo utajikita katika maeneo makuu matano ambapo washiriki watajadili programu zinazolenga kuboresha mifumo ya haki za jinai, kwa kuzingatia kuongeza tija na ufanisi.
Pia utazingatia mifumo ya mashauri ambapo majadiliano yatahusu masuala mbalimbali katika mfumo wa mashauri yakiwemo ya mirathi, ajira na migogoro ya mikataba.
Eneo lingine ambalo litazingatiwa ni migogoro ya wafanyakazi ambapo mkutano huo utachunguza jinsi utatuzi wa mapema unavyoweza kuwanufaisha wafanyakazi na waajiri, kuweka mazingira bora ya biashara na kuvutia wawekezaji katika ukanda wa EAC.
Vilevile mkutano huo pia utahusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika Sheria.