TANZANIA, AU KUUNGANA AJENDA YA NISHATI SAFI

 

TANZANIA, AU KUUNGANA AJENDA YA NISHATI SAFI

TANZANIA, AU KUUNGANA AJENDA YA NISHATI SAFI 

AZERBAIJAN
Umoja wa Afrika (AU) na Tanzania zimeungana katika COP29 nchini Azerbaijan ili kukuza mpango wa nishati safi ya kupikia kama sehemu muhimu ya ajenda ya hali ya hewa duniani. 
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Umoja wa Afrika imeonesha kuwa AU inatambua changamoto ya nishtai safi kama muhimu kwa hatua za hali ya hewa na maendeleo endelevu, iliyosisitizwa kupitia Mpango wake wa nishati safi ya kupikia wa Afrika (ACCP).
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeibuka kama mtetezi mkuu wa nishati safi ya kupikia barani Afrika na hapo awali ilizindua Mpango wa nishati safi ya kupikia kwa Wanawake kupitia COP28 iliyofanyika Dubai na kuhuduhuriwa na Rais Wa Tanzania Dkt Samia na kuhutubia katika majukwaa mbalimbali kwenye mkutano huo na mikutano ya kando.
Aidha Wakati wa COP29, Tume ya Nishati ya Umoja wa Afrika (AFREC) itazindua chapisho, "Uongezaji Endelevu: Kukabiliana na Changamoto ya nishati Safi ya Kupika Barani Afrika," ambalo linatoa ramani ya kina ya kuongeza teknolojia ya katika bara zima la Afrika.