MHE.RAIS DKT SAMIA AWAPONGEZA TAIFA STARS

 

MHE.RAIS DKT SAMIA AWAPONGEZA TAIFA STARS

MHE.RAIS DKT SAMIA AWAPONGEZA TAIFA STARS 

BRAZIL
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewapongeza Taifa STras kufuatia ushindi wa leo Novemba 19 dhidi ya Guinea baada ya kufuzu kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.
Kupitia mitandao yake ya kijamii Mhe Rais Samia ameandika
“Tukiwa katika majonzi na kazi ikiendelea katika kuwatafuta ndugu zetu ambao tunaamini bado wako hai kufuatia kuporomoka kwa jengo eneo la Kariakoo, ninawapongeza vijana wetu Taifa Stars kwa ushindi na kufuzu kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025”
 Pia Mhe.Rais Dkt Samia ameongeza kuwa.
“Mmeandika historia kwa Taifa letu, ikiwa ni mara yetu ya nne kufikia mafanikio haya makubwa katika kipindi cha zaidi ya miaka arobaini. Hongera kwa kazi nzuri nyote tuliowapa dhamana kusimama na vijana wetu kukamilisha jukumu hili katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Benchi la Ufundi na Watanzania wote kwa kuendelea kuipenda, kuithamini na kuipa hamasa Timu ya Taifa”.
Dkt Samia amemaliza kwa kuandika “Baada ya ushindi huu, sasa tujikite katika maandalizi mazuri zaidi kwa mashindano yajayo”.