SERIKALI YAPAISHA BAJETI YA TARURA HADI TSH BIL 710

 

SERIKALI YAPAISHA BAJETI YA TARURA HADI TSH BIL 710

SERIKALI YAPAISHA BAJETI YA TARURA HADI TSH BIL 710

TANZANIA 
Serikali ya awamu ya sita imeongeza bajeti ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara za Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)  kutoka Sh bilioni 275 hadi Sh bilioni  710.
Ongezeko hilo la bajeti ni sawa na  asilimia 158.18 ambapo zinaenda kutekeleza miradi mbalimbali nchini.
Aidha, kutokana na mvua kubwa zilizonyesha maeneo mbalimbali ya nchi na kusababisha madhara makubwa kwenye miundombinu ya barabara kama vile mvua za El nino, kimbunga Hidaya serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali zenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi na mojawapo ya hatua zinazochukuliwa ni kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji.
SOMA HAPA:- Msingi wa maboresho haya ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020 – 2025, kama inavyofafanuliwa katika aya ya 57 ukurasa wa 82.
(Pitia kwenye ilani ya CCM 2020-2025 tafadhali).